f X in
×

Félix Tshisekedi hajawahi kusema atabaki madarakani hadi amani irejee, video hiyo ni deepfake

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado inakabiliwa na hali ya kutokuwa na usalama. Tarehe 1 Julai, video ilisambaa sana mitandaoni ikimuonyesha Rais Félix Tshisekedi akiwa na Mama wa Taifa Denise Nyakeru, kana kwamba anatangaza hana uwezo wa kuandaa uchaguzi na ataendelea kubaki madarakani hadi amani kamili irejee.

Ili kuchunguza video hii, Thibitisha Fact iliwasiliana na msemaji wa Rais, Tina Salama, na kutumia zana maalum kama Google Lens na Hive Moderation kutambua chanzo na kubaini kama ni kazi ya akili bandia.

Baada ya uchunguzi, imebainika wazi kuwa hiyo video ni deepfake. Picha zake ni za mwaka 2020 na hotuba ya uongo iliyotengenezwa kwa AI imeongezwa. Rais hajawahi kusema maneno hayo.

Sikiliza maelezo yote kwenye podcast yetu Thibitisha Habari.

Partager

Avatar photo

Thibitisha Fact se positionne comme une véritable armée numérique dédiée à la lutte contre la désinformation. Nous utilisons une approche multimédia pour atteindre un large public, en produisant des contenus variés tels que des vidéos explicatives, des capsules informatives, des vérifications de faits (fact-checking) et des podcasts. Notre objectif est de sensibiliser et d'éduquer la population sur les dangers des fausses informations, tout en leur fournissant des outils pour naviguer dans un monde médiatique complexe.

Laisser un commentaire

Vous aviez peut-être manqué ceci :